ASHIKIRIWA KWA MAUAJI YA BABA YAKE MZAZI-MULEBA

Kamanda wa polisi mkoani
Kagera Henry Mwaibambe
JESHI la Polisi mkoani Kagera
linamshikilia Issa Sadick (49),
Mkazi wa Itongo tarafa ya
Nshamba Wilaya ya Muleba kwa
tuhuma za mauaji ya baba yake
mzazi na mama yake wa kambo.
Kamanda wa polisi mkoani hapa,
Henry Mwaibambe, amethibitisha
kutokea kwa tukio   hilo lililotokea
juzi majira ya saa 2:45 usiku Kijiji
cha Itongo wilayani humo.
Mwaibambe, alisema Sadick
Hamis (84), aliuwawa kwa
kucharangwa mapanga na kisha
kutenganishwa kichwa na
kiwiliwili wakati mkewe Zamda
Sadick (44), pamoja na
mtoto  wao Juma Sadick (15),
walifariki wakiwa katika hospitali
teule ya Rubya baada ya nao
kucharangwa mapanga.
Alisema familia ya mzee Hamis
ilivamiwa na watu wasiojulikana
wakaanza kuwakata  mapanga na
kumuacha mtoto wao wa kike,
Aza Sadick (19), mwanafunzi wa
shule ya Sekondari Rukondo
kidato cha tatu, bila kumzuru
sehemu yoyote ile na badala yake
walichukuwa simu yake ya
mkononi.
Alisema familia hiyo ilikuwa na
ugomvi wa muda mrefu, kwa
madai kwamba Baba wa familia
hiyo alikuwa akitoa huduma kwa
upendeleo kwa mke wake wa
nne, Zamda.
“Inawezekana kwa sababu Hamis
alikuwa na wake wanne,
yawezekana wake zake wengine
watatu na watoto wao walihisi
kuna dalili ya mke mdogo kupewa
nafasi kubwa ya kurithishwa mali
pamoja na mwanae Juma aliyefia
katika hospatali teule ya Rubya,”
alisema Kamanda Mwaibambe.
Alisema katika mgogoro huo,
mtuhumiwa ndiye aliyekuwa
kinara na ndio maana jeshi la
polisi linamshikilia kwa
mahojiano zaidi.
Zidi kutembelea blog hii kwa habari zaidi/by Sylivester Superius kassa
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment