TAHARIFA YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

Baraza la Mitihani Tanzania
(Necta) limesema usahihishaji
wa mitihani ya kidato cha nne
uliofanyika Novemba mwaka
jana, umekamilika.
Katibu mtendaji wa Necta, Dk
Charles Msonde ameiambia blog yetu
wiki hii kuwa “usahihishaji
umekamilika na baraza lipo
katika uchambuzi wa kuyapanga
na tutakapokamilisha
tutayatangaza”.
Alipoulizwa ni lini hasa matokeo
hayo yatatangazwa, Dk Msonde
alisema: “Tumemaliza
kusahihisha na mchakato wa
kuyapanga ukikamilika
tutawaeleza hivyo msiwe na
shaka.”
Katika kipindi cha miaka miwili
mfululizo, mwaka 2012 na 2013,
Necta ilitangaza matokeo ya
kidato cha nne mwishoni mwa
Februari na mwanzoni mwa
Machi.
Matokeo ya Mtihani wa Kidato
cha Nne uliofanyika mwaka 2013
yalitangazwa Februari 22, mwaka
jana na 2012 yalizua gumzo
kutokana na asilimia 60 ya
watahiniwa kufeli.
Kwa kawaida, muhula wa
masomo kwa kidato cha tano
huanza Julai, huku Machi na
Aprili mchakato wa kuwapangia
shule hufanyika wakati Mei na
Juni hutumiwa kwa maandalizi
kwa wanafunzi hao.
Katika matokeo ya 2013 kama
ilivyokuwa katika matokeo ya
mwaka 2012, shule binafsi
zilikuwa na matokeo mazuri
kulinganisha na za Serikali
zilizokuwa zikitamba miaka ya
nyuma.
Kwa mujibu wa Necta, matokeo
ya mwaka 2013, shule kongwe
za Serikali na zile za vipaji
maalumu, zilishindwa kuingia
kwenye orodha ya shule 30
bora.
Shule kongwe kihistoria
zimekuwa zikitoka kapa katika
matokeo ya Mtihani wa Taifa.
Tofauti na matarajio ya wengi,
shule hizo nyingi hazikuwamo
hata katika orodha ya shule 100
bora.
Baadhi ya shule hizo ni Fidel
Castro ambayo ilishika nafasi ya
83, Malangali (172), Ifunda
Ufundi (205), Jangwani (226),
Bwiru (242), Songea Wavulana
(257), Pugu (325) na Azania
(333).
Ikiwa ni mwaka mmoja
umekamilika tangu Mpango wa
Matokeo Makubwa Sasa (BRN)
ulipoanzishwa, taasisi ya
Hakielimu ilitoa matokeo ya
utafiti wake yanayoonyesha
hakuna kilichofanyika.
Kaimu Mkurugenzi wa HakiElimu,
Godfrey Boniventura alisema
Serikali isitumie kigezo cha
kuongezeka ufaulu kama ishara
tosha ya kuimarika kwa elimu,
kwani licha ya ufaulu huu
kuonyesha kupanda ghafla, kuna
changamoto nyingi katika sekta
hiyo ambazo bado hazijatatuliwa
na juhudi kubwa zinahitajhuu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment