Isikie hii kauli ya mashabiki wa Arsenal kwa nahodha wao wa zamani Cesc Fabregas!!

Vinara wa ligi kuu Engaland wanakutana na wababe wengine wa ligi hiyo Arsenal mwishoni mwa juma hili katika uwanja wa Emirates  ikiwa ni harakati za kuwania ubingwa wa ligi hiyo.
Lakini kauli ya mashabiki wa Arsenal kwa nahodha wao wa zamani Cesc Fabregas ambaye kwa sasa anaichezea Chelsea inaweza kukuchekesha kwani wameutaka uongozi wa klabu hiyo kuondoa bango lenye picha ya staa huyo kwenye uwanja wao.
Mashabiki hao wamesisitizan lazima bango hilo liondolewe kabla ya mchezo wao jumapili kwa kuwa Fabregas anarudi kwenye uwanja huo akiwa mpinzani wao mkubwa.
Fabregas raia wa Hispania aliichezea Arsenal kwa mafanikio makubwa kabla ya kuondoka mwaka 2011 na kujiunga na Barcelona lakini akarejea England na kujiunga na Chelsea ambayo sasa inapambana na Arsenal katika kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England jumapili hii.
Uspitwe na story kama hizi jiunge nasi INSTAGRAM
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment